Jifunze kuhusu Tatizo hili la Kisaikolojia linalopekea mtu kuwa kikwazo cha mafanikio yake yeye mwenyewe
Nini Maana ya "Self-Sabotage?"
Hili ni tatizo la Kisaikolojia ambapo wewe mwenyewe kwa kujua au kutojua (consciously or unconscously) unasimama na kuwa kikwazo cha mafanikio yako mwenyewe. Kwa maana nyingine, kujiharibia wewe mwenyewe. Mfano, unapata kazi nzuri, lakini unaanza kuchelewa au kulewa. Au kuna kazi ya kuapply, unasubiri mpaka deadline ndio unaapply. Mara nyingine, unapata mwenza mzuri, unaanza kumfanyia visa.
Nini chanzo cha tatizo hili?
Watafiti wengi wa mambo ya Saikolojia na nervous system wameeleza vyanzo mbalimbali vya tatizo hili kupitia tafiti zao. Lakini asili ya vyanzo vyote imekuwa ni Experience tunazopitia utotoni.. Experience mbaya za utotoni hudumaza sehemu ya ubongo inayohusika na FIKRA (Neural Pathways to thinking part) na kuimarisha sehemu ya ubongo inayohusika na kujilinda (Neural Pathways to survival). Hizi ni baadhi ya vyanzo vya Self Sabotage;
Wired for Disappointment (Ubongo umejiandaa kufeli)
Hii ni ile hali ambapo ubongo unajitune au kuwa tayari kwa disappointment nafailure muda wote. Hii husababishwa na experience za utotoni. Mfano mzazi anatoa ahadi za uongo kila siku, kama nitakuletea pipi na haleti. Kitu hiki huonekana rahisi kwa mtu mzima sababu ubongo wake umekomaa ila kwa mtoto huumiza. Hivyo ili asiumie tena, ubongo unajiandaa kuwa disappointed. Hali hiyo huendelea mpaka utu uzima. Either kwa kujua au kutojua, unaamua kutojaribu chochote au kufanya ili mradiukiamini wewe ni wa kufeli tu.
Wired for toxic shaming (Ubongo umejiandaa kuaibishwa)
Hii ni ile hali ambapo ubongo unajitune au kuwa tayari kuaibishwa. Hii pia husababishwa na experience za utotoni. Mfano mlezi anakukosoa na kukugombeza kila wakati tena kwa maneno makalikama wewe mjinga, mpumbavu mkubwa, tahira wewe, chizi wewe hivyo ubongo hujiset kuaibishwa. Hata tunapokuwa watu wazima, tunaanza kuhisi kuaibishwa kama tutakosea. Na mara nyingine, huamua kujiaibishwa na kujitukana sisi wenyewe mfano mimi mjinga, sina akili. Hali hii hupelekea kujiharibia sisi wenyewe pale ambapo hatujaaibishwa.
Wired for shot down (Ubongo umejiandaa kujitenga na watu)
Hii ni ile hali ambapo ubongo unajitune au kuwa tayari kujitenga na watu pale unapohisi tatizo. Hii pia husababishwa na experience za utotoni. Mfano mtoto anakosea na mlezi anampiga na kumfungia chumbani. Hali hii ikijitokeza mara kwa mara utotoni, ubongo hujifunza kuji "isolate" kila kunapokuwa na changamoto au task.Ukubwani, unakutana na task kubwa ambayo ingeweza kuchange maisha, unashot down kwa siku kadhaa. Halafu unakuja kujuta, na muda umeshapita.
Utotoni kupewa au kuahidiwa zawadi kwa hata kufanya jambo dogo tu
Wote tunajua zawadi ni motivation kubwa kwa mtoto. Lakini inapozidi, huharibu internal motivation ya kufanya vitu. Zawadi ni external motivation. Ili ubongo wa mtoto ukue vema ni muhimu kumtengenezea vyote External na Internal Motivation.
Mtoto anayekuzwa kwa external motivation tu (kama zawadi), hupungukiwa motivation ya ndani. Hivyo kwenye maisha ya utu uzima, akihisi kitu hakina reward ya moja kwa moja, anasita kufanya au kukifanya vibaya bila kujali. Mfano kazi ofisini.
Adhabu kubwa isiyoendana na umri pale mtoto anapokosea
Kama umekuwa ukipewa adhabu kubwa sana utotoni, ubongo hujitune sehemu ya woga. Hivyo muda mwingi kuogopa kujaribu na kuthubutu kufanya vitu.
Kwenye utu uzima, akili yako huanza kuogopa sana failure kiasi cha kwamba kila nafasi ya kujaribu jambo inapotokea, unajisahaulisha na kutofanya. Hii inaweza kuwa kwa kujua au kutojua.
Nini ufumbuzi wa tatizo hili
Andika experience hasi za utototni na nini unadhani kinaweza kuwa chanzo cha tatizo.
Andika hisia unazokuwa nazo pindi unapotaka kutofanya kitu.
Andika sababu za kutotekeleza mipango yako
Andika sababu zilizofanya ujiharibie kazi
Ondoa mawazo ya kulaumu watu wengine na kuona umerogwa.
Anza kujichunguza kuanzia ndani na kufanya meditation.
Dhamiria kuanza safari ya mabadiliko.
Kama huna kumbukumbu ya nini inaweza kuwa sababu, tafuta msaada wa kisaikolojia.
FOLLOW ME ON INSTAGRAM
Thank